DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO
Rn;Yohana M.Mwazembe Cont:+255764108196
Rn;Yohana Mwazembe
kutokana na changamoto na madhara yanayojitokeza kwa mama mjamzito na mtoto aliyeko tumboni hivyo mwanamke yeyote aliye katika umri wa kuweza kubeba ujauzito,baba familia na jamii kwa ujmla ni vyema kufahamu kwamba dalili na ishara za hatari kipindi cha ujauzito zinaweza kujitokeza wakati wowote usiotarajiwa. Hivyo mama mjamzito anapaswa Kufahamu dalili na ishara zote za hatari zinazoweza kujitokeza wakati wa ujauzito, Kutokana na kutofahamika ni wakati gani dalili ama ishara hizo za hatari zinaweza kujitokeza ni muhimu kufahamu mapema kabla ya kutokea ili kuweza kuchukuwa tahadhari na kufahamu ni kwa namna gani na ni wapi utaweza kupata msaada kabla ya madhara makubwa kujitokeza.
Zifuatazo ni dalili na ishara za hatari kwa mama mjamzito ÷
- kutokwa na Damu ukeni.
- Maumivu makali ya tumbo,kiuno na mgongo.
- Kutokwa na majimaji ukeni.
- Maumivu makali ya kichwa, kuhisi kizunguzungu.
- Macho kushindwa kuona vizuri(kunaona ukungu ukungu).
- Kuvimba uso, mikono na miguu
- Kupoteza Fahamu.
- Kupumua kwa shida/ kifua kubana.
- Kuhisi homa kali/kutapika kupita kiasi.
- Mtoto kupunguza kucheza au kuacha kucheza kabisa.
Endapo utahisi dalili yoyote Kati ya hizo hapo juu chukuwa tahadhari mapema na kwenda hospitali au kituo Cha Afya kilichokaribu yako ili uweze kupatiwa huduma ya haraka, kwani kila dalili ama ishara ya hatari kipindi cha ujauzito inabidi idhibitiwe mapema na kwa haraka ili kuepusha matatizo makubwa yanayoweza kumpata mama ama mtoto aliyeko tumboni.
Matatizo au madhara yanayoweza kujitokeza endapo ishara za hatari hazitadhibitiwa mapema ni pamoja na:-
- Mimba kutoka au kuharibika (abortion/miscarriage).
- Kifafa cha mimba (pre-eclampsia/eclampsia).
- Mtoto kufia tumboni (IUFD).
- Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati kufika (premature baby) chini ya wiki 37 za mimba.
- Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo.
- Mama mjamzito kupoteza maisha
Fahamu kwamba kipindi cha ujauzito ni kipindi ambacho unapaswa kuwa makini Sana katika kufuatilia maendeleo na mabadiliko yanayojitokeza ili kuweza kubaini shida ama changamoto inayoweza kuleta matatizo kwako na kwa mtoto pia.
Asante kwa kusoma makala hii ya Afya ambayo naamini Kuna vitu umeweza kujifunza na ukivizingatia vitaleta matokeo chanya katika safari yako ya kupata mtoto mwenye Afya Bora.
Comments
Post a Comment